Tuesday 12 September 2017

WASANII WANUFAIKA NA ELIMU YA BIASHARA KWA NJIA YA MTANDAO KUTOKA BASATA.



 Katibu mtendaji wa Baraza La Sanaa La Taifa Bw. Godifrey Mungereza akiwa na wataalamu wa masuala ya mtandao, wakwanza kutoka kushoto kwake ni Bw.Sarehe Juma na wa mwisho ni Bw. Michael Mlingwa wakiwa wanasubili kufunguliwa kwa semina hiyo

Katika kukuza na kuendeleza Sanaa hapa Nchini Baraza La Sanaa La Taifa(BASATA) limeendesha semina ya Biashara ya Sanaa kwa njia ya mtandao na sheria inayosimamia sekta ya sanaa kwa wasanii na  vikundi vya sanaa. Semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Baraza La Sanaa La Taifa(BASATA)Kuanzia tarehe 29hadi tarehe 31 Agosti 2017 na wadau mbalimbali wa Sanaa wapatao sitini walihudhuria semina hiyo.

  Semina hiyo iliendeshwa na wataalamu wa masuala ya kimtandao ambao ni Bw.Michael Mlingwa kutoka( social medial) na Bw. Sarehe Juma kutoka (Tanzania House National Tarents) watalaamu hawa waliandaliwa na Baraza La sanaa La Taifa (BASATA) ili kutoa elimu hiyo.Aidha wataalam hawa walianza kwa kufafanua maana ya mitandao ya kijamii ambayo ni jumuiya iliyopo mitandaoni kwa ajali ya kupashana habari, pia walieleza aina mbalimbali ya mitandao ya  kijamii ambayo ni Twiter,Instagram,Facebook,Imo na google.

Walifundisha namna ya kufungua akaunti katika mitandao hii na kuitumia katika kutafuta marafiki kwa lengo la kutaka kupashana habari na kufanya nao biashara mitandaoni walisema”msanii anaweza chonga kinyago na kukipiga picha akatupia mtandaoni na wakaona watu wengi Zaidi”hii usaidia katika kutafuta soko mitandaoni au anaweza tunga wimbo na akawajulisha wadau wake na wakautafuta au kununua.

Aidha wataalamu hao walifundisha namna ya kufanya biashara mitandaoni,” msanii anaweza kufungua akaunti ya Instagram na akatafuta marafiki wengi akatumiwa na makampuni kutangaza biashara zao mfano watu maarufu kama akina Diamond wanatumiwa na makampuni kutangaza biashara zao na kujitengenezea pesa katika akaunti zao”alisema.

Bali na hayo,pia elimu ya sheria zinazo simamia sekta ya sanaa hapa nchini ilifundishwa na Wakiri wa Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA)Bw. Magare.sheria zilizofundishwa ni pamoja na kusajiri kazi zao katika vyombo husika kama Baraza La Sanaa La Taifa( BASATA), Chama cha Hakimiki na Hakishiriki Tanzania(COSOTA), Wakala Wa Usajiri wa Biashara Na lessen(BRELA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania( TRA) alisema kusajili kazi zao husaidia kutambulika kisheria na inakuwa rahisi kuwasaidia wanapohitaji msaada kwani kazi zao zinakuwa zinajulikana.

 Pia hupelekea suala la ulipaji wa kodi jambo ambalo ni uzalendo kwa nchi na huliongezea taifa pato kama Rais anavyo sisitiza kulipa kodi.Wakiri Magare alisema”maisha ya mwanadamu ni uhalisia wa mambo anayofanya sheria ipo ili kulasimisha uhalisia huo”  na pia aliwataka wasanii kufanya sanaa kwa upana  na kwa kushikirikiana na Baraza pia alitumia fursa hiyo kueleza kazi za baraza ambazo ni kusimamia sekta ya sanaa hapa nchini.

Bali na hayo pia, Bw. Mrisho Mrisho(mhasibu wa baraza)alitoa pendekezo kwa wasanii la uanzishwaji wa kuweka mfuko wa mkop kwa wanii(SACCOS)utakaokuwa unawasaidia wasanii kukopafedha ili waweze fanya kazi zao vizuri kwani wasanii wanapata shida pindi wanapohitaji mikopo kutoka kwenye mabenki kutokana na ukweli kwamba sanaa haichukuliwi kama kazi zikingine alisema “inatia aibu wasanii wanapokuwa na matatizo kama magonjwa wanakosa misaada na kufikia hatua ya kupiga magoti kuomba pesa kwa ndugu au jamaa” kwa hiyo tukiwa na saccos yetu mwanachama ataweza kopa na kutatua shida yake pia itasaidia kumaliza tatizo la mtaji .Suala ambalo liliungwa mkono na kalibia kila mwanachama aliyekuwepo katika semina hiyo,aidha wasanii waliomba suala la sacoss litiliwe maanani ili lianzishwekwa mda mfupi ili kuondokana na kero ya mikopo.

Na mwisho mgeni rasimi ambaye alialikwa kuja kuhitimisha semina hiyo Bi  Nsao Viviani Sharua   aliwataka wasanii kutumia elimu waliyoipata katika kazi zao ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na tekinolojia na alisema “tumepanga kukuza sanaa kwa kuwazungukia wasanii huko walipo ili kuwapatia elimu itakayo wasidia katika kazi zao za kisanaa na kuwapa nafasi ya kulijua baraza la sanaa la taifa(BASATA)” na alihitimisha kwa kugawa vyeti kwa walio hudhulia mafunzo hayo.
Bw.Asante Ally mmoja wa wadau waliokuwepo kwenye semina hiyo akiuliza swali kwa mmoja ya wawezeshaji kuhusu namna ya kutafuta marafiki mtandaoni.n
Wadau mbali mbali wakiwa wanafuatilia kwa makini mafunzo kutoka kwa muwezeshaji wa semina hiyo(Aliyekaa katikati ni meneja wa bendi ya msondo ngoma Bw.msumari)
Mgeni rasmi aliyekuwa amealikwa kuhitimisha mafunzo hayo Bi.Nsao Vivian Sharua akigawa vyeti kwa washiriki wa mafunzo hayo na anayepokea cheti ni Bw. Juma Khatibu kutoka kikundi cha nimujo edutainmemt centre.
Bw.Sarehe Juma akiwa anafundisha namna ya kufungua akaunti ya Facebook na namna ya  kuitumia katika kutuma matukio katika mitandao mfano nyimbo,picha kwa lengo la kutangaza biashara kwa kutumia mitandao 

No comments:

Post a Comment