Mwanadada Lilian Loth Lazaro mshindi wa mashindano ya Miss Tanzania Continental
2016/2017 amekabidhiwa rasmi bendera ili kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano ya Miss Africa continental yanayotarajiwa kufanyika Afrika ya
kusini (johannesberg) mwaka huu. Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi ya
katibu mtendaji wa Baraza La Sanaa La Taifa(BASATA) 22/08/2017.
Lilian Loth
alikabidhiwa bendera hiyo baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania
Continental yanayofanyika kila mwaka yakiwa na lengo la kutafuta mshindi
atakaye iwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Africa continental.
Mashindano hayo hujumuisha washindi mbali mabali wanao wakilisha nchi zao, yaani
kila nchi hutoa mshindi mmoja ili ashiriki mashindano hayo na mwisho kumpata
mmoja atakaye wakilisha Afrika katika mashindano ya Dunia.
Mashindao
hayo yalianzishwa tokea mwaka 2014, na hii imekuwa mara ya kwanza Tanzania kutoa
mshiriki katika mashindao haya. Mashindano haya huusisha mwaafrika yeyote
mwenye vigezo vya kutosha kuitambulisha vyema Afrika katika kueneza
utamaduni, mila na desturi za kiafrika.
Mwanadada
Lilian Loth Lazaro mwenye umri wa miaka 22 akitokea chuo kikuu cha kampala university anayesoma shahada ya utawala amekuwa mshiriki wa kwanza kushiriki mashindano
haya hapa nchini baada ya kushinda mashindano ya Miss Tanzania Continental
yaliyofanyika mwaka huu hapa Tanzania.
Aidha katibu
mtendaji wa Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) Bw.Godifrey Mngereza alimkabidhi
bendera hiyo na kumtaka aiwakilishe vyema Tanzania katika mashindano hayo na
alisema ‘nenda ukaiwakilishe vizuri Tanzania na sisi watanzania tupo nyuma yako na
Mungu akubariki’
No comments:
Post a Comment