"Wasanii wengi hapa nchini bado hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii", hayo yalisemwa na Bw.
Magira Werema (Afisa Mikopo kutoka Mfuko
wa hifadhi ya jamii PSPF) tarehe 21 Agosti 2017 alipokuwa kwenye Jukwaa la Sanaa katika viwanja vya
Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) ambapo jumla ya wadau
wapatao sabini (70)
walihudhuria programu hiyo.
Bw. Magira Werema Afisa mikopo kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii
(PSPF) aliwataka wasanii kujiunga na mfuko wa PSPF ili waweze kunufaika
na huduma zinazotolewa na mfuko huo kwani
PSPF wamelenga kusaidia katika majanga
yasiyo kingika kama Magonjwa, Ajari pamoja na Ulemavu. Bw. Werema
alisema “wasanii wengi wanahangaika hasa
wanapopatwa na magonjwa hali ambayo huwalazimu kuomba msaada kutoka serikalini
au kuchangishana wao kwa wao ili waweze kupata matibabu”
ilikuondokana na usumbufu huo akawaomba wasanii wajiunge na PSPF.
Bali na hayo, pia Bw. Magira alieleza mafao
mbalimbali yanayotolewa na PSPF mafao hayo ni Fao la Elimu na Ujasilia
mali, Mafao ya bima ya afya, Fao la uzeeni, Mikopo ya nyumba pamoja na viwanja, pia fao la ulemavu linatolewa, hivyo basi wanachama wake wananufaika na mafao hayo.
Katika Jukwaa hilo, Bw. Augustino Makame kutoka Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) alitowa ombi
kwa PSPF kutafuta namna ya kuwafikia wasanii
hasa waliopo mikoani kwani PSPF haipo kwa ajiri ya wasanii wa Dar es salaam tu, pia aliomba PSPF wawatumie wasanii katika kazi zao hasa
wanapokuwa wanahamasisha watu kujiunga na mfuko huo na wafanyapo mikutano ili kuwainua wasanii.
Bw. Magira Werema mwenye suti nyeusi akiwa na Bw. Augustino Makame kutoka ( BASATA) wakijaribu kuchambua changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau waliokuwepo kwenye Jukwaa hilo. |
Mmoja wa wadau wa sanaa aliyekuwepo kwenye Jukwaa hilo akiuliza swali kwa muwezeshaji hasa juu ya faida za kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF na hatutua za kujiunga na mfuko huo. |
No comments:
Post a Comment