Friday 11 August 2017

MH. DKT. HARRISON MWAKYEMBE AKUTANA NA CHAMUDATA KWENYE UKUMBI WA VIJANA SOCIAL HALL - MWANANYAMALA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati aliyevaa kofia nyeusi) ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye mkutano huu na wanamuziki wa dansi nchini (CHAMUDATA). Kulia ni Kaimu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Onesmo Kayanda, kushoto mwa Waziri ni Mwenyekiti wa CHAMUDATA Bw. Juma Ubao. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa nchini Bi. Joyce Hagu (wa kwanza kushoto) na Katibu Mtendaji wa COSOTA Bi. Doreen Sanare (wa mwisho kulia aliyevaa blauzi ya njano).

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Onesmo Kayanda akiitambulisha meza kuu kwa wasanii wa dansi (hawapo pichani) kwenye mkutano huo wa Mh. Waziri na wanamuziki wa dansi na wadau wa muziki huo nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall uliopo Mwananyamala 'A'

Baadhi ya wanamuziki wa dansi na wadau wao wakifuatilia hoja mbalimbali kwenye mkutano huo kwa makini.



Raisi wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA) Bw. Juma Ubao akiitambulisha hadhira (haipo pichani) kwa Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.


Mwanamuziki mkongwe nchini Kikumbo Mwanza Mpango maarufu kama "King Kiiki" akisalimia hadhira (haipo pichani) kwenye mkutano huo wa Mheshimiwa Waziri na kuhudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki wa dansi nchini.


Wasanii mbalimbali (walioinama) walipokuwa wakijiandikisha kuingia kuhudhuria mkutano huo huku wakisimamiwa vyema na wafanyakazi wa BASATA Bi Flora Mgonja (aliyevaa miwani) na Haidath Tagalile (aliyeshika kiuno).

Sehemu ya wadau na wanamuziki wa dansi nchini waliohudhuria mkutano huo.
Mwanamuziki mkongwe nchini maarufu kama King Malu akionyesha utaalamu wake wa kutumia kifaa cha "saxaphone" mbele ya Mheshimiwa Waziri kwenye mkutano huo.











No comments:

Post a Comment