Katika kukuza na kuendeleza sekta ya Sanaa hapa nchini, kama ilivyo ada Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeendesha semina ya
kuwajengea uwezo wasanii wa kuitumia kibiashara mitandao ya kijamii "social medias". Semina
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa siku tatu kuanzia tarehe
29 hadi tarehe 31 Agosti 2017 na wadau mbalimbali wa Sanaa wapatao sitini (60) walihudhuria semina hiyo.
Semina hiyo iliendeshwa na BASATA kwa kushirikiana na wataalamu wa masuala ya kimtandao kutoka kituo cha Utangazaji cha Clouds Media Group ambao ni Bw. Michael Mlingwa na Bw. Salehe Juma. Aidha wataalam hawa walianza kwa kufafanua maana ya mitandao ya kijamii lakini pia
walieleza aina mbalimbali ya mitandao ya kijamii ambayo mfano Twiter, Instagram, Facebook, Imo, You Tube nk.
Walifundisha namna ya
kufungua/kutengeneza akaunti katika mitandao hii na kuitumia katika kutafuta marafiki kwa
lengo la kutaka kupashana habari na kufanya nao biashara mitandaoni walisema..
”msanii anaweza chonga kinyago na kukipiga
picha akatupia mtandaoni na wakaona watu wengi zaidi tena ndani ya muda mchache tu”.
Mitandao hii inasaidia sana katika
kutafuta masoko ya kazi za wasanii mitandaoni kiurahisi na kwa haraka na kuwafikia watu wengi zaidi.
Aidha wataalamu hao
walifundisha namna ya kufanya biashara mtandaoni, walisema.
”msanii anaweza kufungua akaunti ya Instagram mfano watu maarufu kama
akina Diamond, Alikiba nk wanatumiwa na makampuni kutangaza biashara zao na kujitengenezea
pesa kupitia majina yao”
Na mwisho mgeni rasimi kutoka BASATA ambaye alialikwa kuja kuhitimisha semina hiyo Bi. Nsao Vivian Shalua aliwataka wasanii kutumia
elimu waliyoipata katika kazi zao ili kuendana na mabadiliko ya sayansi na
tekinolojia na alisema
“tumepanga kukuza
sanaa kwa kuwazungukia wasanii huko walipo ili kuwapatia elimu itakayo wasidia
katika kazi zao za kisanaa na kuwapa nafasi ya kulijua baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA)”.
Lakini pia wasanii wote walioudhuria semina hiyo walitambuliwa na BASATA kwa kupewa vyetu vya kuhitimu.
No comments:
Post a Comment