|
Bw. Magira Werema
(Afisa mikopo kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii
(PSPF) akitoa elimu juu ya kujiunga na PSPF kwa wasanii katika viwanja vya Baraza
La Sanaa La Taifa (BASATA) alipokuwa kwenye Jukwaa la Sanaa
|
"Wasanii wengi hapa nchini bado hawajajiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii", hayo yalisemwa na Bw.
Magira Werema (Afisa Mikopo kutoka Mfuko
wa hifadhi ya jamii PSPF) tarehe 21 Agosti 2017 alipokuwa kwenye Jukwaa la Sanaa katika viwanja vya
Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) ambapo jumla ya wadau
wapatao sabini (70)
walihudhuria programu hiyo.
Bw. Magira Werema Afisa mikopo kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii
(PSPF) aliwataka wasanii kujiunga na mfuko wa PSPF ili waweze kunufaika
na huduma zinazotolewa na mfuko huo kwani
PSPF wamelenga kusaidia katika majanga
yasiyo kingika kama Magonjwa, Ajari pamoja na Ulemavu. Bw. Werema
alisema “wasanii wengi wanahangaika hasa
wanapopatwa na magonjwa hali ambayo huwalazimu kuomba msaada kutoka serikalini
au kuchangishana wao kwa wao ili waweze kupata matibabu”
ilikuondokana na usumbufu huo akawaomba wasanii wajiunge na PSPF.
Bali na hayo, pia Bw. Magira alieleza mafao
mbalimbali yanayotolewa na PSPF mafao hayo ni Fao la Elimu na Ujasilia
mali, Mafao ya bima ya afya, Fao la uzeeni, Mikopo ya nyumba pamoja na viwanja, pia fao la ulemavu linatolewa, hivyo basi wanachama wake wananufaika na mafao hayo.
Hivyo basi aliwataka
wasanii wajiunge
na PSPF ili wanufaike
na mafao hayo, kwani wasanii wengi wanahangaika hasa baada ya kuzeeka na hii husababishwa na ukweli kuwa,
muziki una muda wake na hufikia kipindi cha kupumzika hivyo basi wakiwa na PSPF wanaweza kupatiwa fao la uzeeni na kuwasaidia kama wasitaafu wengine wanavyo nufaika na mafao ya uzeeni.
Katika Jukwaa hilo, Bw. Augustino Makame kutoka Baraza La Sanaa La Taifa (BASATA) alitowa ombi
kwa PSPF kutafuta namna ya kuwafikia wasanii
hasa waliopo mikoani kwani PSPF haipo kwa ajiri ya wasanii wa Dar es salaam tu, pia aliomba PSPF wawatumie wasanii katika kazi zao hasa
wanapokuwa wanahamasisha watu kujiunga na mfuko huo na wafanyapo mikutano ili kuwainua wasanii.
Na mwisho Bw. Magira alitowa wito
kwa wasanii kujiunga na PSPF kwani wakati ni sasa na haina haja kubaki
wakihangaika, na alisema hakuna gharama ya kujiunga na mfuko huo, wadau pamoja
nawasanii waliokuwepo kwenye Jukwaa hilo waliitikia wito huo kwakuchukua fomu za kujiunga na mfukohuo kwa wingi,
kwani
elimuiliyotolewa ilionekana kuwahamasisha kujiunga na mfuko huo.
|
Bw.Magira Werema (afisa mikopo kutoka PSPF) akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wadau ikiwa ni pamoja na kuelekeza hatua za kujiunga na mfuko huo, ambapo alisema hakuna ghalama yoyote ile inayotozwa ili kujiunga na PSPF |
|
Bw. Magira Werema mwenye suti nyeusi akiwa na Bw. Augustino Makame kutoka ( BASATA) wakijaribu kuchambua changamoto mbalimbali kutoka kwa wadau waliokuwepo kwenye Jukwaa hilo. |
|
Mmoja wa wadau wa sanaa aliyekuwepo kwenye Jukwaa hilo akiuliza swali kwa muwezeshaji hasa juu ya faida za kujiunga na mfuko wa hifadhi ya jamii PSPF na hatutua za kujiunga na mfuko huo. |
|
Wadau mbalimbali wa
sanaa wakifuatilia kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika mkutano huo.
|