Na mwandishi wetu;
WASANII nchini wametakiwa
kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba katika mifuko mbalimbali ya jamii kwa kuwa
kufanya hivyo kuna kumuhimu mkubwa katika maisha yao baada kuwa wamestaafu kazi
zao au wanapokuwa hawana tena uwezo wa kufanya kazi.
Hayo yalisemwa na msanii
mkongwe wa maigizo hapa nchini Bakari Mbelemba maarufu kwa jina la Mzee Jangala
wakati akizungumza katika Jukwaa la na Sanaa lililofanyika Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) mwanzoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam.
Mzee Jangala alikuwa
akijibu hoja iliyotolewa na msanii Christian Kauzeni ambaye alitaka kujua ni
kwa nini wasanii wakongwe wengi wanakuwa na maisha magumu licha ya kuwa
walifanya kazi nzuri zilizo wajengea umaarufu mkubwa hapa nchini.
Alisema wasanii wengi
wakonge hawakuwa na utaratibu wa kuweka akiba, lakini kwa sasa kuna mifuko
mingi na mifumo mingi ya kujiwekea akiba hivyo ni muhimu kwa wasanii kujiwekea
akiba kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji
wa BASATA, Godfrey Mngereza alisema huu si wakati wa msanii kupata shida baada
ya kustaafu au kuzeeka kwa kuwa kuna mifuko mingi ya kuweka akiba na hata ya
huduma za afya ambayo kwa mchango kidogo inatoa unafuu mkubwa wahuduma.
“Haipendezi kwa msanii
aliyekuwa na jina kubwa au umaarufu katika nchi anapokuwa amepatwa na maradhi
kusubili harambee ipite ili apate matibabu, msanii akijiunga na mfumo wa bima
ya Afya kwa mfano NHIF analipa fedha kidogo sana na anapata uhakika wa matibabu
kwa muda mrefu wa maisha yake,” alisema Mngereza.
Msanii mkongwe Mzee Jangala
(kulia) akiteta jambo na mratibu wa jukwaa la sanaa Rajab Sollo katika jukwaa
la nje jana. Kushoto ni mwenyekiti wa jukwaa hilo Bw. Ernest Biseko.
|
Wasanii wa kikundi cha Mandela Theater Group wacheza ngoma
katika onyesho lao walilofanya kwenye Jukwaa la Sanaa lililofanyika hivi
karibuni katika Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
|
No comments:
Post a Comment