Wednesday, 26 July 2017

WASANII WAASWA KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI ZAO

Mkurugenzi wa kituo cha Utangazaji cha Clouds Bw. Ruge Mutahaba (katikati), kulia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa BASATA Bw. Onesmo Kayanda na kulia ni Mhasibu Mkuu wa BASATA Bw. Mrisho Mtumwa.
 Mkurugenzi wa vipindi kutoka kituo cha utangazaji cha Clouds Bwana Ruge Mutahaba jana kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA) ambapo mada ilikuwa ni Mnyororo wa Thamani (value chain) aliwaasa watanzania kupitia wasanii kuongeza thamani katika kazi zao ili waweze kuongeza ubora wa wanachokizalisha. 

Bwana Ruge alisema...
"Unapotengeneza muziki ukakamilika, kabla ya kuweka bei ya mauzo sokoni ni lazima uuongeze thamani kwa kukumbuka gharama ulizotumia kwa kila hatua uliyopitia katika kuandaa kazi husika, mfano lazima ukumbuke gharama ya producer, studio, muda uliotumia, usafiri nk ili uweze kuwalipa ama kujilipa kwanza kabla ya kuseti bei ya mauzo sokoni".

Sehemu ya umati wa watu walioudhuria jukwaa hilo

Sehemu ya umati wa watu walioudhuria jukwaa hilo

Bwana Ruge Mutahaba akifafanua jambo katika Jukwaa hilo

Monday, 17 July 2017

TANZIA


Tarehe: 17/07/2017


BASATA Arts Centre                                                             Tel. 2863748/2860485
                                                                                                              
Ilala Sharif Shamba                                                                                                                                                                       
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail: info@basata.go.tz

YAH: SALAAM ZA RAMBIRAMBI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mke wa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe Bi. Linah George Mwakyembe aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika Hospital ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. 

Baraza limestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na taarifa ya kifo hiki cha Bi. Linah George Mwakyembe ambaye ukarimu wake hautosahaulika kamwe kwa familia yake lakini pia hata kwa wageni wote ambao walibahatika kufika nyumbani kwa Waziri Mhe. Dr. Harrison Mwakyembe.

Baraza linatoa pole kwa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na familia yote ya marehemu, pia linawatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu. 

Baraza liko pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. Amin.


Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA

Thursday, 13 July 2017

TCRA YAHIMIZWA WASANII JUU YA MATUMIZI SAHIHI YA MITANDAO YA KIJAMII

Naibu Mkurugenzi - Masuala ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Thadayo Joseph Jonas Ringo (katikati) akitoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii katika ukumbi mdogo wa BASATA. Wengine ni Mkurugenzi wa fedha na utawala kutoka BASATA Bw. Onesmo Kayanda na Bi. Agnes Kimwaga (Afisa Habari Mkuu - BASATA).
Kupitia programu ya "Jukwaa la Sanaa" inayo ratibiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambayo hufanywa kila wiki, wasanii mbalimbali jana waliudhuria ili kuweza kufahamu faida na madhara juu ya mitandao ya jamii. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) walitoa elimu kwa wasanii juu matumizi sahii ya mitandao ya kijamii hasa katika zama hizi za sayansi na teknolojia.

Akieleza hayo katika ukumbi mdogo wa BASATA uliopo Ilala Shariff Shamba  muwakilishi kutoka TCRA Bw. Thadayo Joseph Jonas Ringo alisema..
"mitandao ya kijamii itakupa jina, umarufu na faida nyingi sana katika jamii kama ikitumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.., na kwa hakika utaifurahia sana. Lakini pia mitandao hii inakuwa kama shubiri iwapo tutaitumia vibaya kwa malengo ya kiudanganyifu, kuwachafua watu ama kuweka picha zako chafu."
Bw. Ringo akaendelea.
"Na asikudanganye mtu kuwa ukivunja sheria kwa kudanganya jina lako kwenye mtandao eti hatuwezi kukupata, kwa kushirikiana na mamlaka nyingine tutakupata tuu kwa namna yoyote ile, hivi mnajua kuwa mtu akiingia kwenye mtandao (internet) kuna alama zaidi ya elfu moja huwa anaziacha pale!? Hivyo utapatikana tuu na utafikishwa kwenye vyombo vya sheria."

Pamoja na kutoa tahadhari hiyo, bwana Ringo aliendelea kuuelimisha umma wa Watanzania kupitia wasanii kuwa huduma za mitandao ya kijamii ikiwemo simu na kompyuta ni muhimu katika matumizi yetu ya kila siku kimawasiliano, hivyo ingawa teknolojia hii ni mpya na inaendelea kukua aliwataka watumiaji kuzingatia matumizi bora na kufuata sheria za kimtandao.

Pia aliwakumbusha Watanzania kuwa ni muhimu sana kutoa taarifa polisi mara tu utakapoteza simu, kompyuta, laini ya simu ama kifaa chochote ambacho kimebeba taarifa zako ili uweze kujiweka katika mazingira salama kwa lolote litakaloweza kutokea.

Aliongelea pia kuhusu wadukuzi wa akaunti za watu kuwa ni muhimu pia kutoa taarifa mapema kwenye mamlaka husika iwapo akaunti yako unayoitumia kwenye mitandao ya kijamii imeporwa na mtu mwingine. Alimalizia bwana Ringo.

Katibu wa chama cha Ma DJ Tanzania bwana Asanterabi Mtaki (aliyesimama) akitoa ufafanuzi juu ya jambo fulani.
Mwandishi Bwana Ali Thabiti na wenzake wakimhoji mtoa mada Bw.Ringo
Sehemu ya umati wa wasanii mbalimbali waliohudhuria progamu ya Jukwaa la Sanaa mapema jana BASATA

Saturday, 8 July 2017

R.I.P SHABANI DEDE

Baada ya kumaliza mazishi ya mwanamuziki Shabani Dede kwenye makaburi ya kisutu, pia Katibu Mtendaji wa BASATA Bw. Godfrey Mngereza(pichani katikati), wasanii na wadau wengine wa kazi za sanaa walipata wasaa wa kutembelea kaburi la mwanamuziki nguli Marijani Rajabu mbaye alifariki mwaka 1995 na kuzikwa mkaburi ya Kisutu.


Huyu ni mwanamuziki ambaye kazi yake iliwahi kutumika katika mfumo wa elimu ya Sekondari nchini.


Ipo haja ya kurejesha kazi za mwanamuziki Marijani katika mfumo wa elimu ya Sekondari.


Wengine pichani ni Bw. John Kitime (aliyevaa kofia, huyu ni mwanamuziki mashuhuri nchini) na Bw. Msumari (Katibu wa CHAMUDATA).

TANZIA