Wednesday, 18 February 2015

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA ZA WANAMUZIKI JOHN KITIME NA DULLY SYKES




Tarehe: 16/02/2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

BASATA Arts Centre                                                                            Tel. 2863748/2860485
                                                                                                  Fax: 0255- (022) – 286 0486                                                                                                                         
Ilala Sharif Shamba                                                                                                                                                                       
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam

RAMBIRAMBI KWA KIFO CHA MKE WA MWANAMUZIKI JOHN KITIME NA BABA YAKE MSANII DULLY SYKES
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa Bodi ya BASATA Bw. John Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa kuamkia Ijumaa ya Tarehe 13/02/2014.
Aidha, BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa Msanii Dully Sykes, Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe 15/02/2015.
Pamoja na vifo hivi kuacha majonzi na huzuni kwa wanafamilia, ni pigo pia kwenye tasnia ya Sanaa kutokana na ukweli kwamba wote wawili kwa njia moja ama nyingine wamekuwa na mchango katika kuhakikisha tasnia hii inasonga mbele kwa kuwa karibu na wasanii John Kitime na Dully Sykes sawia.
Baraza linatoa pole kwa wadau wote wa Sanaa hususan wasanii na Umoja wa mabloga nchini kwa misiba hii. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu hawa hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey Mngereza
KATIBU MTENDAJI

No comments:

Post a Comment