Tarehe:
16/02/2015
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA Arts Centre
Tel. 2863748/2860485
Fax: 0255- (022) – 286 0486
Ilala Sharif Shamba
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
RAMBIRAMBI KWA KIFO CHA MKE WA MWANAMUZIKI
JOHN KITIME NA BABA YAKE MSANII DULLY SYKES
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha
Mke wa Msanii mkongwe wa muziki wa dansi na Mjumbe wa Bodi ya BASATA Bw. John
Kitime kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa kuamkia Ijumaa ya
Tarehe 13/02/2014.
Aidha,
BASATA linatoa salamu rambirambi kwa kifo cha Baba Mzazi wa Msanii Dully Sykes,
Mzee Abby Sykes kilichotokea jana Jumapili ya Tarehe 15/02/2015.
Pamoja
na vifo hivi kuacha majonzi na huzuni kwa wanafamilia, ni pigo pia kwenye
tasnia ya Sanaa kutokana na ukweli kwamba wote wawili kwa njia moja ama
nyingine wamekuwa na mchango katika kuhakikisha tasnia hii inasonga mbele kwa
kuwa karibu na wasanii John Kitime na Dully Sykes sawia.
Baraza
linatoa pole kwa wadau wote wa Sanaa hususan wasanii na Umoja wa mabloga nchini
kwa misiba hii. Ni matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote
yaliyotendwa na Marehemu hawa hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia
yetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey
Mngereza
KATIBU MTENDAJI