Picha na Dondoo za tukio la Waziri mwenye dhamana na Sanaa
Dkt. Harrison Mwakyembe na Naibu wake Juliana Shonza walipokutana na
Wasanii wa Fani zote tarehe 27/10/2017 kupitia programu yetu ya Jukwaa La Sanaa. Katika
kikao hicho waziri ametolea majibu kero zifuatazo:
1. Suala la muda wa Wasanii wa Muziki katika maenesho yao ambapo kumekuwa na kubanwa muda na kulazimishwa kukatisha maonesho. Waziri amesema tayari ameshazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na tayari kamati imeundwa kupitia sheria ndogo za manispaa zinazokwamisha.
2. Sheria ya hakimiliki na maboresho yake yako katika hatua za mwisho na
ameeleza kwamba ni nzuri na itatatua matatizo ya wizi wa kazi za
Wasanii.
3. Kuundwa kwa Idara za Sanaa katika halmashauri.
Ameeleza ameshazungumza na Waziri mwenye dhamana na TAMISEMI kuhusu
suala hili na linafanyiwa kazi. Ameahidi kulitolea ripoti.
4.
Amezungumzia wasanii kutokaa kimya wanapodhulumiwa haki zao.
Amewataka
kuanza kutumia TEHAMA katika kuuza kazi zao
na kuepuka watu wa kati
ambao wamekua wakifaidika zaidi yao. Ameeleza kufurahishwa na Shirikisho
la Sanaa za Ufundi ambalo tayari limezindua mfumo wa TEHAMA katika
kunadi na kuwafaidisha wasanii wa Sanaa za Ufundi.
No comments:
Post a Comment