Thursday, 10 August 2017

MKUTANO WA MH. DKT. HARRISON MWAKYEMBE NA WASANII WA MUZIKI WA INJILI KATIKA UKUMBI WA NSSF MAFAO HOUSE ILALA, JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati aliyevaa miwani) akisikiliza kwa makini hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wdau wa muziki wa Injili (hawapo pichani). Kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Onesmo Kayanda na kulia mwa Waziri ni Raisi wa Shirikisho la Muziki nchini Bw. Ado November.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Onesmo Kayanda akiongea machache kuhusu BASATA kabla ya kumtambulisha Waziri Mh. Dkt. harrison Mwakyembe kwa wadau wa muziki wa Injili nchini.



Katibu Mtendaji wa Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA) Bi. Doreen Sanare akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa wasanii kusajili kazi zao katika mamlaka husika ili iwe kinga kwao pale yanapotokea matatizo hasa ya kimikataba. 
Raisi wa Shirikisho la Muziki nchini Bw. Ado November akizungumzia changamoto mbalimbali zinazohusu muziki wa injili mbele ya Waziri Mh. Harrison Mwakyembe  kwenye mkutano huo na wanamuziki wa Injili

Baadhi ya wadau walioudhuria mkutano huo
Baadhi ya wadau walioudhuria mkutano huo wakifatilia hoja mbalimbali kwa umakini
Sehemu ya wadau walioudhuria mkutano huo wakifatilia hoja mbalimbali kwa umakini

No comments:

Post a Comment