Friday, 23 December 2016
Wednesday, 14 December 2016
JUKWAA LA SANAA BASATA PALIKUWA HAPATOSHI LEO
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limefanya program yake ya Jukwaa la Sanaa kwa wadau wa sanaa na wa kazi za sanaa.
Mada ya leo ilikuwa:
Fursa za Sanaa Kutokana na Mabadiliko ya Teknolojia
na Dunia ya Utandawazi .
Mtoa mada:
Ruge Mutahaba (Mfanyabiashara, mtunzi na mdau wa muziki).
Ruge Mutahaba (Mfanyabiashara, mtunzi na mdau wa muziki).
Bw. Mutahaba;
Alisema “Sanaa yetu ina mapato mengi kama
serikali kupitia BASATA na mamlaka nyingine husika zikiamua kubadili mfumo
uliopo na kujikita katika mifumo ya sanaa kwa maana ya kibiashara ili mbali na
kukuza vipaji na vipato kwa wasanii mmoja mmoja lakini pia kuongeza pato la
taifa”.
Pia amewashauri “Wasaani kutokana
na mabadiliko ya teknolojia na dunia ya utandawazi, sanaa ni biashara kubwa
kwasasa, hivyo tunapaswa kufahamu na kujua vizuri kuchanganya vionjo mbalimbali vya utamaduni
wetu wa Kitanzania ili kupata ladha inayouzika sokoni hata kimataifa”.
Aidha amewasihi wasanii kuzingatia na kuwa na weledi wa kutosha wa
kutumia mitandao ya kijamii ili kuweza kujitangaza kiurahisi na kwa haraka
lakini pia kufikisha kazi zao kwa jamii kubwa zaidi.
Monday, 12 December 2016
Friday, 2 December 2016
Wednesday, 12 October 2016
Friday, 30 September 2016
BASATA YAMPONGEZA MUSTAFA HASANNALI KWA KUSHINDA TUZO YA UBUNIFU WA MAVAZI
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa nchini linapenda kuchukua
nafasi hii kumpongeza msanii na mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali kwa kushiriki
kinyanga’anyiro cha Tuzo ya Mavazi ya Afrika Mashariki Kenya 2016 (Kenya
Fashion Awards 2016) yaliyofanyika tarehe 03/09/2016 na kupata tuzo ya Mbunifu
Bora wa Mwaka wa Afrika Mashariki.
Baraza linathamini mchango mkubwa wa
Mbunifu huyu wa mavazi katika kuendeleza tasnia ya ubunifu, kwa kuanzisha
Jukwaa la mavazi Afrika Mashariki na Kati, Swahili Fashion week na maonyesho
mengine ya mavazi.
Aidha tuzo hii itakuwa chachu kwa
ustawi wa tasnia ya ubunifu wa mavazi kwa kuwa imedhihirisha ubora wa kazi za sanaa
za Kitanzania katika soko la Kimataifa. Baraza litaendelea kushirikiana na
wabunifu wenye maono na bidii katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini ili
kuhakikisha sekta ya sanaa inasonga mbele kwani ni ukweli usiopingika kuwa
tasnia ya sanaa ina mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa watanzania wengi
hususan vijana.
Baraza linatambua mchango wa Bwana
Mustafa Hassanali katika kukuza maendeleo ya ubunifu na amekuwa akitoa fursa
kwa wabunifu wengine wa Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Baraza
linathamini na linatoa pongezi kwa Bwana Mustafa Hassanali kwa kazi nzuri
anayoifanya.
SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA
Subscribe to:
Posts (Atom)