Baraza la Sanaa la Taifa limepokea
barua toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu ya Tamasha tajwa
linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 20 – 27/9/2015.
Baraza linahimiza vikundi, vyama,
mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonyesha
kazi bora za sanaa.
Aidha, washiriki wote wanatakiwa
kujigharamia wenyewe usafiri wa kwenda na kurudi pamoja na mizigo yao. Nchi
wenyeji itagharamia usafiri wa ndani, chakula, malazi, na matangazo katika
vyombo vya Habari.
Kwa maelezo zaidi unaombwa kufika ofisi
za BASATA, Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko au piga simu namba 0789 094477.
Nakutakia
maandalizi mema.
Imetolewa
na:
Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI
No comments:
Post a Comment