Friday, 6 October 2017

TANZIA

Mzee Mchoya Mtaki Malogo 
Baraza la Sanaa la Taifa linasikitika kutangaza kifo cha msanii mkongwe wa ngoma za asili za Kigogo na kiongozi muanzilishi wa kikundi cha Nyati Utamaduni Group, Mzee Mchoya Mtaki Malogo kilichotokea tarehe 04/10/2017 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili saa sita usiku.

Mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa leo saa kumi kwenda Mkoani Dodoma kwa ajili ya mazishi. Safari ya kusafirisha mwili wa marehemu itaanzia hospitali ya Lugalo

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho tarehe 07/10/2017 saa kumi jioni katika kijiji cha Nzali, kata ya Chilonwa, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. 

Baraza lina wapa pole wanafamilia na wasanii wote kwa msiba huu.

Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.