Thursday 18 June 2015




TANGAZO KWA WASANII WOTE

YAH: MWALIKO WA KUSHIRIKI TAMASHA LA UTAMADUNI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JAMAFEST – 2015

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu.

Baraza la Sanaa la Taifa limepokea taarifa ya mwaliko kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuwa Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajiwa kufanyika nchini Kenya, jijini Nairobi, kwa siku 8 kuanzia tarehe 2 – 9 Agosti, 2015.

Tamasha hili litahusisha mambo mbalimbali ikiwemo Sanaa za jukwaani, Maonesho ya bidhaa mbalimbali za Kiutamaduni, Warsha na kongamano, Michezo na Sanaa za Watoto, Kutembelea vivutio asilia na vya Utamaduni na Soko la Tamasha la kuuzia bidhaa za kiutamaduni.

Baraza linahimiza vikundi, vyama na mashirikisho ya sanaa, wasanii na wadau wa sanaa kutumia fursa hii kuonesha kazi bora za sanaa za Kitanzania.

Aidha, washiriki watapaswa kujigharamia usafiri wa kwenda na kurudi hadi Nairobi, Malazi, chakula wakati wote wa Tamasha, tiba na bima.

Kwa maelezo zaidi unaombwa kufika Ofisi za BASATA, Idara ya Ukuzaji Sanaa na Masoko au piga simu namba 0789 094 477

Nakutakia maandalizi mema.

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI



Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mtendaji
All correspondence to be addressed to The Executive Secretary
BASATA Arts Centre, Ilala Sharif Shamba, P.O. Box. 4779, Dar es Salaam, Tanzania.
Telephone: 2863748/2860485, Fax: 0255 – (022) 286 0486 E-mail: basata06@yahoo.com Website: basata.or.tz


No comments:

Post a Comment