Tarehe: 02/03/2015
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
BASATA Arts Centre
Tel. 2863748/2860485
Fax: 0255- (022) – 286 0486
Ilala Sharif Shamba
P.O. Box. 4779, Dar es Salaam
E-mail:
basata06@yahoo.com
SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA
MHESHIMIWA CAPTAIN JOHN DAMIAN KOMBA (MB)
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha
Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Captain John
Damian Komba kilichotokea jioni ya Jumamosi ya tarehe 28/02/2015.
Captain
John Damian Komba ni msanii na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini.
Amekuwa ni taa na nuru ambayo katika kipindi chote cha uhai wake imeangaza na
kutoa mwanga angavu kwenye sekta ya Sanaa.
Mchango
wake katika muziki wa dansi, kwaya na ule wa kiweledi katika kuandaa na kukuza
wasanii mbalimbali nchini hautasahaulika kamwe. Ni mdau aliyeacha alama kuu
katika muziki wa bendi, kwaya na taarabu na amejitolea kwa kiasi kikubwa katika
kuufikisha muziki wa dansi na kwaya mahali ulipo leo.
Aidha,
pamoja na kujiunga na siasa na hatimaye kuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga
Magharibi, Mheshimiwa Komba hakukoma kuendelea kuipigania sekta ya Sanaa kwani
alikuwa ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii ambayo kwa
mujibu wa kanuni za Bunge ndiyo inayoisimamia na kuishauri Serikali katika
masuala yote yahusuyo sekta ya Sanaa na Utamaduni.
Baraza,
wasanii na wadau wote wa Sanaa hatuna budi kuendelea kuenzi mema yote aliyotuachia
marehemu John Komba hasa katika kutunga nyimbo za hamasa na ujumbe makini na
wenye mashiko kwa jamii yote ya Watanzania.
Hakika
pengo lililoachwa na Marehemu haliwezi kuzibika, kwani imekuwa ni kama mshumaa
uliyozimika ghafla wakati tukiingia kwenye giza.
Baraza
linatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne
Makinda, wabunge na wadau wote wa Sanaa hususan wasanii kwa msiba huu. Ni
matumaini ya Baraza kwamba, tutaendelea kuenzi mema yote yaliyotendwa na Marehemu,
hasa kudumisha upendo na amani katika tasnia yetu ya Sanaa na taifa kwa ujumla.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Amen
Godfrey
Mngereza
KATIBU MTENDAJI
Marehemu Mhe. Capt. John Komba enzi za uhai wake |